Additional information
ISBN | 979-8-89248-515-9 |
---|---|
Author | Daniel Mburu Mwangi |
Publisher | |
Publication year | |
Language | |
Number of pages | 106 |
Kitabu hiki kinahusu usimilishaji wa ishara za isimu katika Breili. Mada hii imetafitiwa kwa mujibu wa malengo manne ya utafiti. Kwanza, mtafiti alilenga kuchanganua rasimu ya Breili ya Kingereza na ile ya Kiswahili. Pili, mtafiti alidhamiria kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili ya Kiswahili. Tatu, utafiti huu ulidhamiria kufafanua […]
ISBN: 979-8-89248-515-9
€37.99
ISBN | 979-8-89248-515-9 |
---|---|
Author | Daniel Mburu Mwangi |
Publisher | |
Publication year | |
Language | |
Number of pages | 106 |
Kitabu hiki kinahusu usimilishaji wa ishara za isimu katika Breili. Mada hii imetafitiwa kwa mujibu wa malengo manne ya utafiti. Kwanza, mtafiti alilenga kuchanganua rasimu ya Breili ya Kingereza na ile ya Kiswahili. Pili, mtafiti alidhamiria kubainisha na kutatua changamoto zinazozuia usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili ya Kiswahili. Tatu, utafiti huu ulidhamiria kufafanua namna ukosefu wa ishara za kiisimu huathiri ufundishaji wa isimu na lengo la nne lilikuwa kubainisha namna mikato ya Breili ya Kiingereza na ile ya Kiswahili inaathiri uchapishaji wa vitabu vya isimu.
Sura ya kwanza imeshughulikia hisgtoria fupi ya maandishi ya breili na asili yake. Sura ya pili nayo imeangazia vikwazo katika ufundishaji na usomaji wa breli, uchopekaji wa michoro na picha katika breili, na ufaafu wa teknolojia katika breili.
Sura ya tatu imeangazia athari inayosababishwa na kuwepo kwa rasimu mbalimbali za Breili kama vile rasimu ya Kiingereza, rasimu ya Kiswahili 1978 na ile ya 1995. Pia imechunguza vikwazo vinavyojitokeza katika uchanganuzi wa sentensi za lugha.
Sura ya nne nayo imeangazia vikwazo vinavyodumaza usimilishaji wa ishara za kiisimu katika Breili ya Kiswahili.