Home » Product » UJUMI MWEUSI NA UNUSURA WA FASIHI YA KISWAHILI: NYIMBO ZA MUZIKI WA DANISI WA TANZANIA

UJUMI MWEUSI NA UNUSURA WA FASIHI YA KISWAHILI: NYIMBO ZA MUZIKI WA DANISI WA TANZANIA

Ujumi Mweusi na Unusura wa Fasihi ya Kiswahili: Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania, ni kitabu kinachoelezea kwa kinagaubaga suala la unusura katika fasihi ya Kiswahili, mifano ikitolewa kutoka nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Kimsingi, zipo kazi za kifasihi zinazodumu kwa muda mrefu bado zikiwa zinaendelea kuwa na dhima kuntu kwenye jamii […]

ISBN: 979-8-89248-922-5

27.99

Additional information

ISBN

979-8-89248-922-5

Author

Elihaki Yonazi

Publisher

Publication year

Language

Number of pages

79

Description

Ujumi Mweusi na Unusura wa Fasihi ya Kiswahili: Nyimbo za Muziki wa Dansi wa Tanzania, ni kitabu kinachoelezea kwa kinagaubaga suala la unusura katika fasihi ya Kiswahili, mifano ikitolewa kutoka nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania. Kimsingi, zipo kazi za kifasihi zinazodumu kwa muda mrefu bado zikiwa zinaendelea kuwa na dhima kuntu kwenye jamii yake. Hali hii ndiyo inayofahamika kama unusura. Fasihi ya Kiafrika, ikwemo ile ya Kiswahili dhima yake kuu ni ya kijamii, kama vile; kufunza, kukosoa, kuadabisha na kuhifadhi lugha. Kama kazi ya fasihi kwa mtazamo wa Kiafrika, itajitenga na dhima hiyo, haitakuwa na tija katika jamii yake, hivyo itakosa unusura.

Kazi za kifasihi kama vile, riwaya Kusadikika (Shaaban Robert) na nyimbo za muziki wa dansi wa Tanzania, kama vile Mtaa wa Saba (Mwinshehe Mwijuma), ni miononi mwa kazi chache za fasihi ya Kiswahili zenye unusura. Yapo maswali mengi yanayoweza kuulizwa, kwa nini kazi hizi zimedumu kwa muda mrefu? Je, ni mapenzi ya watu kwenye kazi hizi au ni msuko wa kazi zenyewe? Kitabu hiki kimejaribu kujibu maswali haya.