Home » Product » Mikabala Ya Waandishi Wa Vitabu Vya Kiada Kuhusu Mtindo Wa Uandishi Insha Za Kiswahili Katika Shule

Mikabala Ya Waandishi Wa Vitabu Vya Kiada Kuhusu Mtindo Wa Uandishi Insha Za Kiswahili Katika Shule

Vitabu vya kiada vina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya. Licha ya umuhimu huu katika mchakato wa ufundishaji na ujifundishaji, vitabu vya kiada huwasilisha mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha na hivyo, kuwatatiza walimu na wanafunzi wanaovitumia. Kazi hii iililenga kuchunguza mikabala ya uandishi wa […]

ISBN: 979-8-89248-700-9

35.99

Category:

Additional information

ISBN

979-8-89248-700-9

Author

Nester Ateya

Publisher

Publication year

Language

Number of pages

105

Description

Vitabu vya kiada vina nafasi kubwa katika ufundishaji na ujifundishaji wa insha za Kiswahili katika shule za upili nchini Kenya. Licha ya umuhimu huu katika mchakato wa ufundishaji na ujifundishaji, vitabu vya kiada huwasilisha mikabala tofauti kuhusu mtindo wa insha na hivyo, kuwatatiza walimu na wanafunzi wanaovitumia. Kazi hii iililenga kuchunguza mikabala ya uandishi wa vitabu vya kiada na mchango wake kwa ufundishaji na ujifundishaji wa mtindo wa insha za Kiswahili. Utafiti uliongozwa na madhumuni mahsusi yafuatayo: kubainisha mikabala mbalimbali ya waandishi wa vitabu vya kiada kuhusu ufundishaji na ujifindishaji wa mtindo wa insha. Nadharia ya Mtindo iliyoasisiwa na Milic Louis (1965) ilitumika kwa kuzingatia mihimili ya ubinafsi na muundo. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa kithamano, muundo ukiwa wa kimaelezo. Utafiti ulifanywa katika eneo la Kaunti ndogo ya Mumias Magharibi, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya. Utafiti uliwalenga walimu wa Kiswahili na wanafunzi wote wa kidato cha kwanza hadi cha nne wa shule za upili kaunti ndogo ya Mumias Magharibi. Sampuli ya utafiti iliteuliwa kitabakishi, kimaksudi na kinasibu. Walimu 22 na wanafunzi 320 walishirikishwa.